al-Fawzaan kuhusu kitabu cha Ibn-ul-Qayyim “ar-Ruuh”

Swali: Mtu huyu anauliza kuhusu Kitaab “ar-Ruuh cha Ibn-ul-Qayyim na kama kuna makosa na anayeanza hafai kukisoma?

Jibu: Ndio. Kina faida kubwa na utafiti. Na pia kina mambo ambayo yanatakiwa kutazamwa. Mwanafunzi anayeanza asikisome. Ambaye anaweza kukisoma ni yule aliye thabiti na achukue ya faida humo na aache ambayo yanatakiwa kutazawa. Yasemekana ya kwamba ndio kitabu cha kwanza alichoandika Ibn-ul-Qayyim kabla ya kukutana na Shaykh wake [Ibn Taymiyyah]. Yasemwa hivi na Allaah anajua zaidi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=v3pZBObHxQo
  • Imechapishwa: 05/06/2022