Vipi kukichinjwa katika ´Aqiyqah vichinjwa vitatu au vinne?

Swali: Vipi kukichinjwa katika ´Aqiyqah vichinjwa vitatu au vinne?

Jibu: Sunnah ni vichinjwa viwili. Lakini watu wakiwa wengi na havitoshi, vile vyenye kuzidi havizingatiwi kuwa ni ´Aqiyqah. ´Aqiyqah ni vichinjwa viwili. Vichinjwa zaidi ni kwa ajili ya wageni. Sunnah ni vichinjwa viwili peke yake kwa ajili ya mtoto wa kiume na kichinjwa kimoja kwa ajili ya mtoto wa kike. Lakini wageni wakiwa wengi, kukiwemo majirani na wengineo, na akaona kuwa vichinjwa viwili haviwatoshi, hapana neno akazidisha kichinjwa cha tatu kwa ajili ya wageni. Lengo ni kuwakirimu wageni.

Swali: Vipi kichinjwa kimoja kikichinjwa sasa na kingine wakati mwingine?

Jibu: Hapana vibaya na hakuna neno. Kichinjwa kimoja kinaweza kuchinjwa baada ya siku saba na kingine baada ya siku mbili, baada ya mwezi au baada ya mwaka kutegemea na uwezo na wepesi wa hali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23609/هل-تجوز-الزيادة-فوق-ذبيحتين-في-العقيقة
  • Imechapishwa: 06/03/2024