Swali: Je, makanisa yanampasa imamu ni mamoja ilikuwa kabla ya kutekwa au baada ya kutekwa?

Jibu: Wanapoteka mji na ikiwa walikutwa na kanisa basi yatabakizwa ikiwa sio katika kisiwa cha kiarabu kama vile Shaam, ´Iraaq na maeneo mengine. Watabakiziwa makanisa yao. Haja ikipelekea kuswali ndani yake inafaa kuswali ndani yake. Mfano wa haja ni kunyesha kwa mvua na jua kali. Hapana neno kuswali ndani yake haja ikipelekea kufanya hivo. Hata hivyo mtu asiswali kwa kuelekea picha. Aswali upande wa kulia mwa picha au upande wake wa kushoto.

Swali: Je, tunaweza kujenga kanisa kwa ajili ya manufaa fulani?

Jibu: Hapana. Wasijenge kanisa jipya. Bali yatabaki tu yale makanisa yao ambayo yalikutwa.

Swali: Wakisilimu?

Jibu: Wakisilimu watayaondoa. Lakini yatabaki yale makanisa walionayo ambayo wanayalipia kodi.

Swali: Ikiwa hakuna mnaswara aliyebaki?

Jibu: Ikiwa hakuna mnaswara aliyebaki hawatoyabakiza. Watayageuza kuwa majumba au kitu kingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23627/حكم-الكناىس-في-بلاد-الاسلام
  • Imechapishwa: 06/03/2024