Swali 54: Ni kipi bora kujifunza elimu au kulingania kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala)?

Jibu: Kujifunza elimu kwanza. Kwa sababu mtu hawezi kulingania kwa Allaah kama hana elimu. Akiwa hana elimu basi hawezi kulingania kwa Allaah. Akifanya hivo basi ataharibu zaidi kuliko atakavyopatia:

قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ أَنَا وَمَنِ اتَّبَعَنِي ۖ وَسُبْحَانَ اللَّـهِ وَمَا أَنَا مِنَ الْمُشْرِكِينَ

“Sema: “Hii ndio njia yangu: nalingania kwa Allaah, juu ya ujuzi na umaizi – mimi na anayenifuata. Utakasifu ni wa Allaah na mimi si miongoni mwa washirikina.”[1]

Yako mambo ambayo yako wazi ambayo mtu wa kawaida anaweza kulingania kwayo kukiwemo kuswali. Anaweza vilevile kukemea kitendo cha kuacha kuswali kwa mkusanyiko. Aidha kuwalingania familia yake na kuwaamrisha watoto kuswali. Mambo haya yako wazi na anayatambua mtu wa kawaida na mwanafunzi. Lakini mambo yanayohitaji uelewa na utambuzi, mambo ya halali na haramu, Tawhiyd na shirki, ni lazima mtu awe na elimu.

[1] 12:108

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 145-146
  • Imechapishwa: 06/03/2024
  • taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy