Swali: Vipi kuhusu Zakaat-ul-Fitwr?

Jibu: Zakaat-ul-Fitwr ni pishi ya chakula inayotolewa na mtu wakati anapomaliza Ramadhaan. Sababu yake ni mja kuonyesha furaha juu ya kula kwa kumaliza Ramadhaan. Kwa ajili hii ndio maana ikaitwa Zakaat-ul-Fitwr au Swadaqat-ul-Fitwr. Inawajibika pale ambapo jua litazama usiku wa kuamkia ´iyd. Lau mtu atazaa mtoto usiku wa kuamkia ´iyd baada ya jua kuzama hatolazimika kumtolea Zakaat-ul-Fitwr yake. Katika hali hii itakuwa imependekezwa tu. Kadhalika ikiwa mtu atakufa kabla ya jua kuzama usiku wa kuamkia ´iyd haitolazimika kumtolea Zakaat-ul-Fitwr. Amekufa kabla ya kupatikana sababu ya uwajibu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/257)
  • Imechapishwa: 20/06/2017