Swali: Ni ipi hukumu ya Zakaat-ul-Fitwr?

Jibu: Zakaat-ul-Fitwr ni faradhi iliyofaradhisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifaradhisha Zakaat-ul-Fitwr kuwa pishi ya tende au pishi ya shayiri kwa kumaliza Ramadhaan.”

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifaradhisha Zakaat-ul-Fitwr ili imsafishe aliyefunga kutokamana na maneno ya upuuzi na kauli chafu na kuwalisha masikini.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/258)
  • Imechapishwa: 20/06/2017