Amekumbuka kutoa Zakaat-ul-Fitwr baada ya kuswali ´iyd

Swali: Kuna mtu alimpa baba yake Zakaat-ul-Fitwr aitoe lakini hata hivyo akasahau mpaka baada ya kuswali ´iyd kisha ndio akaitoa. Je, inazingatiwa na kuna kinachomlazimu?

Jibu: Baada ya swalah ya ´iyd inazingatiwa na katika hali hiyo inakuwa swadaqah ambayo ni lazima kuitoa. Haijalishi kitu hata baada ya kuswali ´iyd inakuwa katika dhimma yake na ni wajibu kuitoa. Ikiwa amekusudia kuchelewesha anapata dhambi pamoja na uwajibu wa kuitoa. Ikiwa hakukusudia isipokuwa alisahau au haikumuwia rahisi kuitoa anatakiwa vilevile kuitoa na hapati dhambi. Muhimu ni kwamba ni lazima kuitoa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/14891
  • Imechapishwa: 20/06/2017