Swali: Leo kuna ugumu wa kupata fariki asiyekuwa na chakula cha siku. Nimeona katika jumuiya moja ar-Riyaadh wengi wanaopokea Zakaat-ul-Fitwr ni watu walio na chakula cha mwezi au mwaka mzima. Je, inafaa watu kama hawa kuwapa Zakaat-ul-Fitwr?

Jibu: Hakuna yeyote aliyesema kuwa Zakaat-ul-Fitwr hapewi isipokuwa yule asiyekuswa na chakula cha mchana au usiku mzima. Hakuna yeyote aliyesema hivi. Zakaat-ul-Fitwr anapewa fakiri. Zakaat-ul-Fitwr ni yule asiyekuwa cha cha kumtosheleza kwa muda wa mwaka. Huyu ndiye fakiri. Huyu ndiye anayepewa Zakaat-ul-Maal na Zakaat-ul-Fitwr. Wale walioshurutishiwa kuwa na chakula cha mchana na usiku mzima ni wale wanaostahiki kutoa na sio wale wanaostahiki kupewa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/4586
  • Imechapishwa: 20/06/2017