Swali: Je, ni sahihi ya wanayosema baadhi ya waislamu kuwa viongozi wa waislamu ni katika mawalii wa Allaah hata kama watakuwa watenda maovu wakubwa?

Jibu: Maneno haya si sahihi. Fasiki ni fasiki ni sawa akiwa ni katika viongozi waliotangulia au waliokuja nyuma au wengine. Walii, sawa ikiwa ni katika zama za hapo kale au zitazokuja nyuma, bado ni walii. Zama hazibadilishi sifa za mtu, uwalii wake wala ufuska wake. Mawalii wa Allaah ni wale wenye imani na taqwa. Amesema (Ta´ala) katika Suurah Yuunus:

“Tanabahi! Hakika mawalii wa Allaah hawana khofu juu yao na wala hawatohuzunika. Ambao wameamini na wakawa wana taqwa.”

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/389)
  • Imechapishwa: 24/08/2020