Swali: Je, inajuzu kuapa kwa Qur-aan na kuapa kwa asiyekuwa Allaah?

Jibu: Inajuzu kuapa kwa Qur-aan kwa kuwa ni maneno ya Allaah. Maneno Yake ni sifa miongoni mwa sifa Zake (Ta´ala).

Ama kuhusu kuapa kwa asiyekuwa Allaah haijuzu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuapa kwa asiyekuwa Allaah amefanya shirki.”

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/235-236)
  • Imechapishwa: 24/08/2020