Swali: Je, inajuzu kuswali kwenye msikiti ambapo kumezikwa maiti kutokana na udharurah wa kutokuwepo msikiti mwingine pamoja na kujua kuwa ikiwa sintoswali kwenye msikiti huu basi sintoswali mkusanyiko na Ijumaa?

Jibu: Ni wajibu kuliondosha kaburi la huyo aliyezikwa humo na kulipeleka makaburini na kumzika huko. Haijuzu kuswali ndani ilihali kaburi liko ndani yake. Ni wajibu kwako kutafuta msikiti mwingine uweze kuswali Ijumaa na mkusanyiko kiasi na utakavyoweza.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/267)
  • Imechapishwa: 24/08/2020