Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali kwenye msikiti ulio na makaburi na makuba?

Jibu: Haijuzu kwa muislamu kuswali kwenye msikiti uliojengwa juu ya makaburi. Msingi wa hilo ni dalili zenye kuonesha makatazo ya kujenga misikiti kwenye makaburi. Moja katika hizo ni ile iliyothibiti katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ya kwamba Umm Salamah alimweleza Mtume wa Allaah kuhusu kanisa aliloliona Uhabeshi na mapicha [masanamu] yaliyokuwemo ndani ambapo akawa amesema:

“Hao ni viumbe waovu kabisa mbele ya Allaah.”

Nyingine ni ile iliyopokelewa na Ahl-us-Sunan kupitia kwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ambaye amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi, wale wenye kufanya ni mahala pa kuswali na wenye kuyawekea mataa.”

Imethibiti katika “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy na Muslim kupitia kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah awalaani mayahudi na manaswara, wameyafanya makaburi ya Mitume wao kuwa ni mahala pa kuswalia.”

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/267-268)
  • Imechapishwa: 24/08/2020