Swali: Ni ipi hukumu ya kujenga misikiti kwenye makaburi na ni ipi hukumu ya kuibomoa?

Jibu: Haijuzu kujenga misikiti kwenye makaburi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kufanya makaburi ni mahapa pa kuswali na amemlaani mwenye kufanya hivo. Hilo linahusu kujenga misikiti kwenye makaburi na kuswali ndani yake.

Msikiti ukijengwa kwenye makaburi ni wajibu kuubomoa. Kwa sababu msikiti huo umeasisiwa kinyume na njia ya Kishari´ah. Sababu nyingine kubakia kwenye msikiti huo na kuswali ndani yake ni njia inayopelekea katika shirki.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/272)
  • Imechapishwa: 24/08/2020