Swali: Watu wa mji wetu wamebomoa msikiti ili waujenge upya. Msikiti huu ulikuwa umejengwa juu ya kaburi. Baada ya kuanza ujenzi walirudisha jengo hilo kwenye kaburi lile na hawakuliweka nje ya msikiti. Ni ipi hukumu ya kujitolea kwa msikiti huu na inajuzu kuswali ndani yake baada ya kuujenga kwenye kaburi kwa vile kaburi liko kwenye chumba na mlango wake wa kuingilia unapitia msikitini?

Jibu: Ikiwa hali ya mambo ni kama ulivyosema haijuzu kujitolea kujenga msikiti huu wala kushiriki katika kuujenga. Vilevile haijuzu kuswali ndani yake. Bali lililo la wajibu ni kuubomoa.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (1/272)
  • Imechapishwa: 24/08/2020