Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya kinyango cha moyo kwa ajili ya kukumbuka uwezo wa Allaah (´Azza wa Jall)?

Jibu: Picha ya moyo au viungo vingine vya mwili sio katika picha zilizoharamishwa, kwa sababu ni baadhi ya sehemu yake. Kwa msemo mwingine inafaa kuchora moyo, mkono, mguu au kichwa – bi maana kila kiungo kimoja kivyake. Hata hivyo tatizo ni kutumia pesa katika mambo kama haya. Manufaa yanayopatikana katika picha hayalingani wala hata kukaribia na zile pesa zinazotumika. Kwa hivyo kutumia pesa katika vitu kama hivi ni jambo linahitaji kuangaliwa vizuri. Kwa hivyo salama zaidi ni kuepuka.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/341)
  • Imechapishwa: 02/05/2026