Kuhusiana na vijana wetu waliopakwa mchanga wa machoni sisi tunawafanyia upole na kuwapa udhuru. Lakini hata hivyo tunachotaka kutoka kwao wakimbie kwa haraka kurejea katika haki na wajue kuwa wamedanganywa. Hakuna mwingine aliyewadanganya isipokuwa ni Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal. Ninaapa kwa Allaah wamewadanganya na kuziharibu akili zao na kuwageuza kuwa sanaa na kucheza na mikono yao. Waheshimu uanaume wao. Waheshimu mfumo wao. Watambue kuwa katika hali hiyo wako katika batili na kwamba ni katika wanusuraji wa batili mpaka pale watapotubu kwa Allaah na kurejea katika mfumo wa Ahl-ul-Hadiyth ambao ndio kundi lililonusuriwa, Twaaifat-un-Mansuurah. Huu ndio mfumo uliyopo hapa nchini tokea takriban miaka mia mbili na khamsini au miaka mia tatu ya nyuma. Allaah ameunufaisha Uislamu na waislamu kwa mfumo huu. Ummah unasubiri kutoka kwenu kuinyanyua bendera ya Tawhiyd na Sunnah ambayo ilibebea Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum), Taabi´uun, Ahmad bin Hanbal, Ibn-ul-Qayyim na Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab. Sio bendera ya Sayyid Qutwub ambaye anazungumza kwa Wahdat-ul-Wujuud, maneno ya kipuuzi, Bid´ah na upotevu. Jepesi lililo kwake ni Takfiyr. Jepesi lililo kwenye fikira za Sayyid Qutwub ni kuukufurisha Ummah. Hili ndio jambo bora alilo nalo. Hili peke yake linamtosheleza kumuweka katika safu za Khawaarij. Hili ndio jepesi kabisa lililo kwa Sayyid Qutwub. Vipi basi atafanywa kuwa ni Imaam na Mujaddid? Watu waliomzunguka ni wanajeshi wanaomtetea na kutetea vitabu vyake, fikira zake na mwelekeo wake wa kupinda.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kutoka kitabu “Firqat-un-Naaniyah – Misingi na I´tiqaad zake”
  • Imechapishwa: 27/08/2020