Leo tuhuma zimekuwa ni za kisiasa. Hapo kale tuhuma zilikuwa ni za kuhusu ´Aqiydah. Lakini hii leo tuhuma zimekuwa ni za kisiasa na wakati huo huo zimeambatana na mambo ya ´Aqiydah. Wanasema kuwa wanachuoni wetu ni wajinga na hawafahamu mambo ya kisasa, fataawaa zao hazifai, ni wenye kuwapaka mafuta watawala na matusi tele. Haya ndio yaliyokuwa yakisemwa na Khawaarij. Khawaarij walikuwa wakiwatuhumu Maswahabah na wakiona wao ndio wako katika haki. Upande mwingine Maswahabah hawajui haki na wala hawaelewi Uislamu! Leo kunafanywa hayohayo.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kutoka kitabu “Firqat-un-Naaniyah – Misingi na I´tiqaad zake”
  • Imechapishwa: 27/08/2020