Swali: Kuna bwana mmoja yeye na mke wake wana kafara ya kiapo. Je, azikusanye na kuzitoa kwa pamoja?

Jibu: Kiapo kimoja anatakiwa kuwalisha chakula masikini kumi. 

Swali: Ampe mmoja au kumi?

Jibu: Awape masikini kumi. Awatafute hata kama watakuwa magharibi au mashariki mwa ulimwengu.

Swali: Awakusanye?

Jibu: Si lazima kuwakusanya. Anaweza kumlisha mmojammoja. Mmoja anaweza kumpa leo, mwingine akampa mapema, mwingine ´Aqabah, mwingine  ar-Riyaadh, mwingine nje ya nchi na mwingine Howtat.

Swali: Ina maana kwamba kafara ya kiapo kimoja inatosha kwa mfano juu ya viapo viwili au viapo vitatu?

Jibu: Inatosha ikiwa ni juu ya kitu kimoja hata kama viapo aliapa mara vingi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22970/حكم-جمع-عدة-كفارات-يمين-وكيفية-اخراجها
  • Imechapishwa: 26/09/2023