Swali: Ni jambo linalotambulika ya kwamba wanazuoni wanatofautiana katika elimu yao. Wako watu wanaosema kuwa elimu inachukuliwa kutoka kwa wakubwa tu na wanaachwa wadogo ingawa wengi katika wanafunzi ni wadogo.

Jibu: Chukua elimu kwa yule ambaye una yakini kuwa ana elimu, ni mamoja ni mkubwa, ni mdogo au ni wa katikati. Chukua elimu kutoka kwa wastahiki wake. Watu walikuwa wakichukua elimu kutoka kwa wenye nayo. Ibn ´Abbaas alikuwa ni miongoni ni Maswahabah wadogo sana. Wajumbe walikuwa wakimjia na wakichukua elimu kutoka kwake licha ya kwamba walikuwepo Maswahabah wakubwa kama mfano wa ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf, az-Zubayr bin ´Awwaam, al-Haarith bin ´Ubaydillaah na wengineo. Tunachotaka kusema ikijulikana kuwa kijana anayo elimu basi inachukuliwa elimu kutoka kwake. Elimu ya Shari´ah ni yale aliyosema Allaah na Mtume Wake.

Swali: Kuhusiana na swali lililotangulia wanatumia dalili kwa Hadiyth inayosema kuwa kujifunza elimu kutoka kwa wadogo ni katika alama za Qiyaamah.

Jibu: Hapana, haina msingi. Sijui kuwa ina msingi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22969/هل-يوخذ-العلم-من-الاكابر-والاصاغر
  • Imechapishwa: 26/09/2023