7 – Anas amesimulia:

”Mjakazi mmoja ambaye ´Umar alikuwa amemtambulisha kwa baadhi ya Wahajiri na Wasaidizi alikuja kwake. Alikuwa amevaa jilbaab ambapo akamuuliza: ”Je, umeachwa huru?”Mwanamke yule akajibu: ”Hapana.” Akasema: ”Vipi mbona jilbaab? Iondoe kutoka kichwani mwako. Hakika jilbaab ni juu ya wanawakwe wa kiumini waungwana.” Alipokawia kufanya hivo akasimama na kumpiga katika kichwa chake kwa mjeledi mpaka akaiondoa kutoka kichwani mwake.”[1]

[1] Ibn Abiy Shaybah katika “al-Muswannaf”: ´Aliy bin Mushir ametuhadithia, kutoka kwa al-Mukhtaar bin Fulful, kutoka kwa Anas bin Maalik.

Cheni yake ya wapokezi ni nzuru na ni kwa mujibu wa sharti za Muslim. Haafidhw Ibn Hajar ameisahihisha katika “ad-Diraayah fiy Takhriyj Ahaadiyth-il-Hidaayah”. Ibn Abiy Shaybah na ´Abdur-Razzaaq katika “al-Musannaf” wameipokea pia kupitia kwa Qataadah, kutoka kwa Anas ambaye amesema:

”´Umar alimuona kijakazi amejifunika kwa jilbaab ambapo akampiga na kusema: ”Usijifananishe na wanawake waungwana.”

Haafidhw Ibn Hajar amesema:

”Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh.”

Ni kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim.

Ibn Abiy Shaybah pia ameipokea kupitia kwa az-Zuhriy, kutoka kwa Anas. Cheni hiyo ya wapokezi ni Swahiyh pia. Imaam Muhammad ameipokea kupitia kwa Ibraahiym kwamba:

”´Umar bin al-Khattwaab alikuwa akiwapiga wajakazi wanaovaa jilbaab na kuwaambia: ”Msijifananishe na wanawake waungwana.” (al-Aathaar, uk. 39)

Cheni hii ya wapokezi inakosa wasimulizi wawili kwa kufuatana, lakini zinatosha zile cheni mbili za wapokezi zilizoungana kutoka kwa Anas. Baadaye nikapata cheni ya wapokezi ya nne katika ”as-Sunan” ya Sa´iyd bin Mansuur.

Kinachokusudiwa hapa ni kwamba ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) alimjua kijakazi huyu licha ya kuwa alikuvaa amejifunika kwa jilbaab. Hiyo inaleta maana ya wazi kabisa kuwa uso wake ulikuwa wenye kuonekana, vinginevyo asingemjua. Mambo yakishakuwa hivo, basi maneno yake:

”Msijifananishe na wanawake waungwana.”

ni dalili ya wazi kabisa kuwa ´Umar alikuwa anaona kuwa miongoni mwa sharti za jilbaab sio kufunika uso. Endapo wanawake wote katika wakati huo walikuwa wanajifunika nyuso zao kwa jilbaab basi ´Umar asingelisema hivo. Kwa hivyo upokezi huu ujumuishwe na mapokezi yaliyotangulia kutoka kwa mwanawe ´Abdullaah, Ibn ´Abbaas na ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhum) yanayosema kuwa uso sio uchi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 99-100
  • Imechapishwa: 26/09/2023