30. Mtume alifanya nini baada ya kutoka kwake Thaqiyf?

Swali 30: Alifanya nini (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) baada ya hapo?

Jibu: Wakati wa misimu na mikusanyiko ya watu alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwaomba watu wamlinde ili aweze kufikisha ujumbe wa Mola wake. Hatimaye Allaah akawapa wajumbe kutoka katika Wanusuraji wasimamie jukumu hilo. Wanusuraji walikuwa kundi la Mwingi wa rehema na kikosi cha imani.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 102
  • Imechapishwa: 26/09/2023