Swali: Ni ipi hukumu mume kumdanganya mke wake?

Jibu: Katika mambo yanayohusiana na mambo yao; inafaa kwake mke kumdanganya mume na inafaa kwake mume kumdanganya mke.

Swali: Vipi?

Jibu: Katika mambo yanayowahusu wao wawili; naapa kwa Allaah nitakununulia kitu fulani, naapa kwa Allaah sikufanya kitu fulani. Mfano mwingine mke akimuuliza kama amefanya kitu fulani ambapo akamdanganya kuwa hakufanya jambo ambalo linaweza kumshawishi. Kwa mfano mke akamuuliza mume kama alienda kuchumbia, akamuuliza kama alikesha kwa mke mwingine na kwamba anamwendea zaidi kuliko anavyomjia yeye na mfano wa hayo.

Swali: Inaa kwake kuapa kwa jina la Allaah?

Jibu: Inafaa kwake kuapa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22358/ما-حكم-الكذب-بين-الزوجين
  • Imechapishwa: 10/03/2023