Kumswalia Mtume katika Tasahhud ya mwisho kwa kifupi

Swali: Wakati wa kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) nilisema:

اللهم صلِّ على محمدٍ

“Ee Allaah! Msifu Muhammad.”

Sikumswalia Mtume kikamilifu.

Jibu: Swalah yake ni sahihi. Lakini ameacha kinachotakikana. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoulizwa aliwaambia waseme:

قولوا: اللَّهم صلِّ

“Semeni: “Ee Allaah! Msifu… “

Hakuna kitu kinachofahamisha ulazima wa kufanya hivo. Lakini kwa minajili ya kuchukua tahadhari zaidi mtu aisome katika Tashahhud ya mwisho na imesisitizwa kufanya hivo na kwa ajili ya kutoka nje ya makinzano ya wanazuoni:

Swali: Kwa hivyo ni faradhi kusema:

اللهم صلِّ على محمدٍ

“Ee Allaah! Msifu Muhammad.”

peke yake?

Jibu: Mtu anatakiwa kuisoma juu ya hali na sifa yake:

اللهم صلِّ على محمدٍ، وعلى آل محمدٍ، كما صليتَ على آل إبراهيم، وبارك على محمدٍ، وعلى آل محمدٍ، كما باركتَ على آل إبراهيم

“Ee Allaah! Msifu Muhammad, jamaa zake Muhammad kama ulivyowasifu jamaa zake Ibraahiym, mbariki Muhammad na jamaa zake Muhammad kama ulivowabariki jamaa zake Ibraahiym… “

Akikusanya kati ya jamaa za wawili hao ndio bora zaidi kwa kusema:

محمد وآله، وإبراهيم وآله

“Muhammad na jamaa zake, Ibraahiym na jamaa zake… “

Swali: Je, ni wajibu au nguzo?

Jibu: Kikosi cha wanazuoni wanaona kuwa ni nguzo, kikosi kingine wanaona kuwa ni wajibu na kundi la tatu wanaona kuwa inapendeza. Lakini kwa hali yoyote mtu hatakiwi kuiacha katika Tasahhud ya mwisho kwa ajili ya kutoka nje ya makinzano.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22369/حكم-الصلاة-على-النبي-في-التشهد-بغير-الوارد
  • Imechapishwa: 10/03/2023