Ameleta Takbiyr ya kwenda katika Rukuu´ kisha akarudi nyuma

Swali: Kuna mtu aliingia ndani ya swalah peke yake, kisha akasoma al-Faatihah na baada yake akasoma baadhi ya Aayah kutoka ndani ya Qur-aan. Lakini hata hivyo akasahau baadhi ya Aayah ambapo akasema “Allaahu Akbar” kwa kuashiria kwa mikono na mdomo kama vile anataka kurukuu, lakini akazikumbuka Aayah alizosahau na akaendelea katika hali ya kusimama na akazikamilisha. Ni ipi hukumu ya swalah yake?

Ibn Baaz: Hakurukuu?

Muulizaji: Hapana. Udhahiri ni kwamba aliashiria tu, lakini alipiga Takbiyr kwa mikono na ulimi wake.

Jibu: Maoni ya karibu zaidi – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kwamba hakuna kinachomlazimu. Kwa sababu hakurukuu. Kurukuu kunakuwa kwa kitendo na si kwa maneno peke yake.

Swali: Kwa hivyo alete Takbiyr mara nyingine baada ya kumaliza kusoma Aayah?

Jibu: Ndio, alete Takbiyr na arukuu.

Swali: Asujudu sujuud ya kusahau akinyanyua mikono yake?

Jibu: Hapana, kunyanyua mikono hakuwajibishi sujuud ya kusahau. Kwa sababu alinyanyua kwa nia ya Rukuu´ kisha hakuikamilisha Rukuu´ yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22332/ما-حكم-من-كبر-للركوع-ثم-رجع-للقراءة
  • Imechapishwa: 10/03/2023