Ute wa manjano na kahawia ni alama ya kusafika kwa mwanamke

Swali: Je, ute wa manjano na kahawia huwa ni alama ya kusafika kwa mwanamke ikiwa damu imesimama?

Jibu: Ikiwa ataona ute wa manjano baada ya kusafika, hana jukumu lolote. Alama hiyo ni kama mkojo. Katika hali hiyo anachotakiwa kufanya ni kutamba kwa maji na kutawadha wakati wa kila swalah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/27561/هل-الكدرة-والصفرة-تكون-علامة-للطهر
  • Imechapishwa: 12/04/2025