Katika hali hii inafaa kwa mwanamke ndani ya eda kutoka

Swali: Mwanamke anayemkalia eda ndugu yake anatakiwa asitoke nyumbani?

Jibu: Anaweza kutoka, anaweza kubaki nyumbani na anaweza kuvaa mavazi mazuri kwa muda wa siku tatu.

Swali: Anafanya kazi shuleni?

Jibu: Anaweza kutoka kwenda shuleni. Atoke kwa ajili ya mahitaji yake. Haya ni miongoni mwa mahitaji – atoke kwa ajili ya kufundisha, akiwa mfanyakazi au mwanafunzi; haya ni miongoni mwa mahitaji. Lakini bila kujipamba wala kutumia manukato.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/27562/حكم-خروج-المراة-من-البيت-فترة-الاحداد
  • Imechapishwa: 12/04/2025