Usiwaingiza watoto katika shule za makafiri za kimagharibi

Swali: Muulizaji kutoka Ufaransa anauliza kama inafaa kumpeleka mtoto wake katika shule za kifaransa kwa sababu anakhofia asije kupotea kwa kuzurura mitaani? Anakusudia kwamba anachelea juu yake asije kujifunza baadhi ya maneno ya barabarani na hivyo anauliza kama inafaa kumuanzisha shule ili ajifunze khaswa kwa kuzingatia kwamba katika masomo hayo wanawafunza msingi wa Tawhiyd.

Jibu: Haijuzu. Amuhifadhi nyumbani kwake. Amlinde nyumbani kwake au atafute kituo cha Kiislamu. Ufaransa na Uingereza kuna vituo vingi vya Kiislamu.

Swali: Vingi katika hivyo wanatoza ada ili watoto kuanza shule?

Jibu: Akijitahidi basi Allaah atamfanyia wepesi jambo lake:

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ

“Na yeyote yuleanayemcha Allaah, atamjaalia njia [ya kutoka katika matatizo] na atamruzuku kutoka njia ambayo hatizamii.” (65:02-03)

Allaah atamfanyia wepesi ambaye atamuhurumia na kumkubalia.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23313/كيف-تكون-تربية-ابناء-المسلمين-في-الغرب
  • Imechapishwa: 25/12/2023