Swali: Tuna mwalimu anayekata ndevu zake na anasema kuwa inafaa kufanya hivo akijengea hoja kwa maneno ya Imaam ash-Shaafi´iy.

Jibu: Anasihiwe. Hakuna yeyote ana haki ya kutia neno lake katika Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Punguzeni masharubu na ziacheni ndevu; wakhalifuni washirikina.”

Swali: Je, ash-Shaafi´iy anasema kuwa inafaa kukata ndevu?

Jibu: Haijalishi kitu. Afunzwe mtu huyo. ash-Shaafi´iy na mwengine yeyote sio hoja katika kwenda kinyume na Sunnah. Si ash-Shaafi´iy wala mwengine yeyote.

Swali: Wanasema kuwa wanazuoni kama vile Shaykh Ibn Baaz na Ibn ´Uthaymiyn wanajengea hoja kwa maneno ya Imaam Ahmad.

Jibu: Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anaposema jambo mambo kwisha. Ahmad wala mwengine yeyote hana nafasi.  ash-Shaafi´iy wala mwengine yeyote hana nafasi. Ibn ´Abbaas amesema:

“Mnakaribia kuteremkiwa na mawe kutoka mbinguni. Nawaambie yale yaliyosemwa na Mtume wa Allaah na nyinyi mnanambia yale yaliyosemwa na Abu Bakr na ´Umar?”[1]

Utamlinganisha wapi Abu Bakr na ´Umar pamoja na ash-Shaafi´iy na Ahmad? Abu Bakr na ´Umar ni watukufu zaidi kuliko ash-Shaafi´iy, Ahmad, Abu Haniyfah na Maalik. Ibn ´Abbaas aliwakemea wakati walipoenda kinyume na Sunnah kwa sababu eti ya maneno ya Abu Bakr na ´Umar.

[1] Ahmad (3121) na wengineo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23312/ما-الرد-على-من-يجيز-الاخذ-من-اللحية
  • Imechapishwa: 25/12/2023