Usimwagi maji ya Moto ardhini kabla ya kusema “Bismillaah”

Swali: Baadhi ya watu kabla ya kumwaga maji ya moto wanasema “Bismillaah” na wanasema kuwa wanachelea yasimwagikie jini na hivyo akaja kuniudhi. Je, maneno haya ni sahihi?

Jibu: Ndio. Usiweke kitu kizito wala maji ya moto mpaka kwanza useme “Bismillaah” ili jini liweze kujitenga mbali. Wanajitenga mbali wasifikwe na jambo. Unapotaja jina la Allaah wanakimbia na hivyo hawafikwi na kitu. Ama usipotaja jina la Allaah unaweza ukawapata na jambo na wao wakaja kukuvamia na kulipiza.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (41) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-3-15.mp3
  • Imechapishwa: 20/08/2020