Usichafue mazulia ya msikiti na viatu vyako

Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali na viatu?

Jibu: Hapana vibaya. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiswali na viatu.

Swali: Je, ni kwenda kinyume na mayahudi?

Jibu: Ndio, amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Swalini na viatu vyenu. Jitofautisheni nao.”

Lakini watu wengi hawajali misikiti iliyotandikwa mazulia na wanayachafua. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliswali na viatu na aliswali bila ya viatu. Hilo khaswa pale ambapo mtu anakhofia kuchafua msikiti… kwa sababu wengi ni wajinga na hawajali.

Swali: Kwa hivyo haina neno mtu akaswali na viatu na akaswali peku?

Jibu: Hapana neno. Ikiwa msikiti umetandikwa mazulia asiyachafue na kuwafanya watu kuikimbia misikiti.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22957/ما-حكم-الصلاة-بالنعال
  • Imechapishwa: 25/09/2023