46. Mwanamke mwenye upara kwenye nyusi zake

4 – Qabiyswah bin Jaabir amesema:

”Kuna mwanamke ambaye tulikuwa tunamfunza Qur-aan. Akaondoka pamoja na wanawake wengine watatu wazee kutoka katika Banuu Asad kwenda nyumbani kwa Ibn Mas´uud. Alipoona nyusi zake zenye upara akasema: ”Unazinyoa?”Mwanamke yule akasema: ”Anayenyoa nyusi zake ni mke wako.” Akasema: ”Ingia ndani. Ikiwa anafanya hivo basi mimi sina lolote kuhusiana naye.” Akaingia ndani kisha akarudi na kusema: ”Naapa kwa Allaah! Sijamuona akifanya hivo.” ´Abdullaah bin Mas´uud akasema: ”Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla ´alayhi wa sallam) akisema:

“Allaah amemlaani mwanamke mwenye kuchanja [kufanya tattoo] na mwenye kuchanjwa, mwanamke mwenye kutoa nyusi na mwenye kutolewa nyusi, mwanamke mwenye kuchonga meno na mwenye kuchongwa meno na mwenye kubadilisha maumbile ya Allaah kwa ajili ya kupata uzuri.”[1]

[1] Cheni yake ya wapokezi ni nzuri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 98
  • Imechapishwa: 25/09/2023