3 – ´Imraan bin Huswayn amesema:

”Wakati nilipokuwa nimekaa pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuja Faatwimah (Rahimahaa Allaah) na akasimama mbele yake. Akamtazama. Alikuwa mweupe sana usoni mwake. Akasema: ”Sogea karibu, ee Faatwimah.” Akasogea karibu mpaka aliposimama mbele yake. Akaweka mkono wake shingoni mwake na kusema: ”Ee Allaah! Ambaye unamshibisha mwenye njaa na Mwenye kuondoa unyonge! Usimfanye Faatwimah, msichana wa Muhammad, kupatwa na njaa.” Nikamtazama na kuona jinsi inavyorudi rangi ya uso wake. Ukaondoka ule umanjano uliokuwa usoni mwake. Baada ya hapo nikakutana naye na kumuuliza juu ya hilo akasema: ”Bado sijahisi njaa tena, ee ´Imraan.”[1]

[1] Ibn Jariyr katika “at-Tahdhiyb” na ad-Duulaabiy katika ”al-Kunaa”. Cheni yake ya wapokezi haina neno kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 97-98
  • Imechapishwa: 25/09/2023