2 – Abus-Sulayl amesema:

”Msichana wa Abu Dharr alikuja na huku amevaa sketi mbili mbaya za sufi na mashavu yamepakwa rangi. Mkononi alikuwa na kikapu. Msichana huyo akasimama mbele yake na yeye alikuwa na marafiki zake ambapo akasema: ”Baba kipenzi! Wakulima na wapandaji wanadai kuwa unyonge huu unakufilisi.” Akasema: ”Msichana kipenzi! Kiweke chini. Kwani hakika baba yako amekuwa – na himdi zote ni zake Allaah – hamiliki dhahabu wala fedha isipokuwa hiki kinamfilisi.”[1]

[1] Ibn Sa´d na Abu Nu´aym katika “al-Hilyah”. Cheni yake ya wapokezi ni nzuri kupitia zingine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 97
  • Imechapishwa: 25/09/2023