Swali 28: Wakati gani (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alienda Thaqiyf na ilikuweje?

Jibu: Alipofariki ami yake Abu Twaalib ndipo washirikina wakasimama kidete na kumuudhi (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwelikweli. Hivyo akaenda Thaqiyf akiwalingania kwa Allaah na kuwaomba wamlinde na wamnusuru ili aweze kufikisha ujumbe wa Mola wake. Hakuna watu waliomkabili vibaya zaidi na kumuudhi kama wao. Walifikia mpaka kuwachochea watoto wao wakamtupia mawe mpaka visigino vyake vitukufu vikaanza kuvuja damu[1]. Mara baada ya kurudi Makkah alikimbilia kwa al-Mutw´im bin ´Adiy[2].

[1] Ibn Ishaaq, uk. 263

[2] al-Bukhaariy (3139).

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 100-101
  • Imechapishwa: 24/09/2023