Fawziy al-Bahrayniy na Haddaadiyyah wananituhumu kuwa naona kwamba matendo ni sharti ya kukamilika kwa imani (شرط الكمال), ikiwa na maana kwamba nayaondosha matendo katika imani.

Ni miongoni mwa uwongo na uzushi mkubwa kabisa. Mimi namwabudu Allaah kwa kuona kuwa matendo ni sehemu katika imani. Mimi nilikuwa miongoni mwa wa mwanzo kukaripia ibara kama “matendo ni sharti ya kukamilika kwa imani” (شرط الكمال) na “matendo ni sharti ya kusihi kwa imani (شرط الصحة). Nalingania katika yale yaliyothibitishwa na Ahl-us-Sunnah ya kwamba imani ni maneno, matendo na ´Aqiydah na matamshi mfano wa hayo yaliyopokelewa kwa mapokezi mengi kabisa kutoka kwa Ahl-us-Sunnah. Wanayajua hayo kwangu licha ya hivo wananikanushia nayo. Kadhalika al-Bahyrayniy hapa anakanusha kwamba mimi natamka waziwazi kwamba matendo ni tanzu ya imani, ikiwa na maana kwamba ni sehemu katika imani, inayoikamilisha imani, bi maana sehemu yake inayoikamilisha.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kashf Akaadhiyb wa Tahriyfaat wa Khiyaanaat Fawziy al-Bahrayniy, uk. 126-127
  • Imechapishwa: 24/09/2023