Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Fikisheni kutoka kwangu ijapo Aayah moja tu.”

Je, hili linamuhusu mwanafunzi peke yake?

Jibu: Hapana, wengine pia. Kila muumini anaweza kufikisha ijapo Aayah moja. Linamuhusu mwanafunzi na kila muumini.

Swali: Baadhi ya watu wanaifahamu Hadiyth hiyo kama ilivyo. Matokeo yake wanatoka kwenda vijijini na katika miji na wanawalingania watu kisha wanajiingiza katika kutoa fatwa kubwakubwa, jambo ambalo pengine likawatia katika matatizo.

Swali: Ni sawa akitoka na kuwafunza watu Qur-aan. Lakini haijuzu kwake kujiingiza ndani ya mambo yasiyomuhusu. Haijuzu kwake kuzungumzia elimu ilihali hana utambuzi. Lakini anaweza kuwafunza Qur-aan, al-Faatihah, zile Suurah za kati na kati na Allaah atamjaza kheri kwa hilo. Kufunza Qur-aan ni jambo jepesi ingawa hana elimu. Awafunze Qur-aan. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mbora wenu ni yule aliyejifunz Qur-aan na akaifunza.”

Tulijifunza Qur-aan kupitia watu wasiojua chochote katika elimu. Hata hivyo tulisoma kutoka kwao Qur-aan tukiwa wadogo. Kuna kheri na baraka kwao – Allaah awasamehe. Walikuwa na subira katika kufunza na katika kuwaongoza watu ingawa hawakuwa na elimu. Lakini walikuwa na subira katika kuwafunza watu Qur-aan, kuwarudiliarudilia na kuwaelewesha nayo mpaka wakaihifadhi. Hili ni jambo limewekwa katika Shari´ah. ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mbora wenu ni yule aliyejifunz Qur-aan na akaifunza.”

“Fikisheni kutoka kwangu ijapo Aayah moja tu.”

Swali: Aayah hapa kumekusudiwa hekima au Aayah za Qur-aan?

Jibu: Aayah za Qur-aan.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22968/معنى-بلغوا-عني-ولو-اية-ومن-المكلف-بها
  • Imechapishwa: 25/09/2023