Swali 29: Ni lini majini walisikia Qur-aan? Hayo yalitokea maeneo gani?

Jibu: Hayo yalitokea katika kilimo cha mitende kati ya Makkah na at-Twaaif wakati alipokuwa njiani akirejea kutoka Thaqiyf. Miongoni mwa waliyosikia ni Suurah ”ar-Rahmaan”:

فَبِأَيِّ آلَاءِ رَبِّكُمَا تُكَذِّبَانِ

”Basi ni zipi katika neema za Mola wenu mnazikadhibisha?”[1]

wakasema: ”Hatukadhibishi chochote katika neema Zako, ee Mola wetu. Ni Zako himdi zote njema.”[2]

Allaah akateremsha juu ya hilo:

وَإِذْ صَرَفْنَا إِلَيْكَ نَفَرًا مِّنَ الْجِنِّ يَسْتَمِعُونَ الْقُرْآنَ فَلَمَّا حَضَرُوهُ قَالُوا أَنصِتُوا ۖ فَلَمَّا قُضِيَ وَلَّوْا إِلَىٰ قَوْمِهِم مُّنذِرِينَ

”Wakati Tulipowaelekeza kwako kundi miongoni mwa majini wakisikiliza Qur-aan, walipoihudhuria walisema: “Nyamazeni [msikilize]!” Ilipokwisha [kusomwa], waligeuka kurudi kwa watu wao wakiwaonya.”[3]

قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا

“Sema: “Nimefunuliwa Wahy ya kwamba kundi miongoni mwa majini lilisikiliza, wakasema: “Hakika sisi tumeisikia Qur-aan ya kushangaza .”[4]

[1] 55:13

[2] at-Tirmidhiy (3291) na al-Haakim (2/473).

[3] 46:29

[4] 72:1

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 101
  • Imechapishwa: 25/09/2023