Swali: Kuna wanaosema kuwa haina neno kuwa na rafiki ambaye ni Shiy´iy au myahudi kwa kutumia hoja ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimtembelea kijana wa kiyahudi.

Jibu: Alimtembelea kwa ajili ya kumlingania katika dini ya Allaah na akamwambia:

“Shuhudia ya kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah.”

Akamwangalia kwanza baba yake ilihali anataka kukata roho. Baba yake kijana akamwambia:

“Msikilize Abul-Qaasim.”

Ndipo yule kijana akasema:

“Nashuhudia ya kwamba hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah.”

 Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akawaambia Maswahabah zake:

“Mshughulikieni ndugu yenu.”

Kwa kuwa ameingia katika Uislamu. Mtu kama huyu anasimamiwa na waislamu katika kumuosha, kumvika sanda, kumswalia na kumzika. Alimtembelea kwa ajili ya kumlingania katika Uislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir%20ayat-03-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 21/06/2020