Swali: Pindi ninapomlingania baba yangu (ambaye ni mjinga katika baadhi ya mambo) katika mambo fulani huanza kunifanyia mzaha na kunifanyia kiburi na hakubali kitu kutoka kwangu. Natakiwa kuchukua msimamo gani?

Jibu: Puuzia haya. Mlinganie baba yako na mnasihi. Muombe Allaah amwongoze. Kariri mashauri yako kwa upole na ulaini. Usifanye ukali na ugumu. Usikate tamaa. Utamwacha baba yako katika upotevu? Hapana, usimwache. Mwangalie Ibraahiym (´alayhis-Salaam) alivyokuwa kwa baba yake. Hakumwacha isipokuwa baada ya yeye kujua kuwa ni adui wa Allaah. Alipojua kuwa ni adui wa Allaah ndipo akamwacha:

وَمَا كَانَ اسْتِغْفَارُ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ إِلَّا عَن مَّوْعِدَةٍ وَعَدَهَا إِيَّاهُ فَلَمَّا تَبَيَّنَ لَهُ أَنَّهُ عَدُوٌّ لِّلَّـهِ تَبَرَّأَ مِنْهُ

“Na haikuwa Ibraahiym kumuombea maghfirah baba yake isipokuwa kwa sababu ya ahadi aliyoahidiana naye. Lakini ilipombainikia kwamba yeye ni adui wa Allaah, alijiepusha naye.” (09:114)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (26) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir%20ayat-03-08-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 21/06/2020