Umekosa kazi nyingine muhimu ya kufanya?

Swali: Ni ipi hukumu ya kutazama mechi za mpira kwenye TV?

Jibu: Umekosa kazi nyingine mpaka unatazama mechi za mpira kwenye TV? Muislamu wakati wake ni wenye thamani. Hatakiwi kuupoteza kwenye mechi, vipindi vinavyoendelea na vitu vingine vya machukizo ambavyo havimpi manufaa katika dini wala dunia yake. Auchunge wakati wake katika mambo yanayomnufaisha na kumpa faida. Bora kwako ni wewe kulala kuliko kutazama mechi. Bora kwako ni kulala, ukapumzika na ukaamka kuswali mwishoni mwa usiku kuliko kutazama mambo yasiyokuwa na faida, vikakucheleweshea kulala na kukufanya kuhisi uvivu juu ya swalah ya Fajr.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=iEMwbTkQPps
  • Imechapishwa: 13/08/2023