Swali: Kuhusiana na mafuta ya mzeituni ambayo yanatoka katika mti uliobarikiwa. Je, mtu atibu uchawi kwayo?

Jibu: Mzeituni unatokana na mti uliobarikiwa. Mtu atibu yale yaliyojaribiwa kuwa yananufaisha. Yote ni kheri. Ni dawa nzuri na mtu atibu kwayo yale yaliyojaribiwa kuwa yananufaisha.

Swali: Mtu ajipake mafuta yake na kuyanywa?

Jibu: Yote ni sawa kujipaka mafuta yake na kuyanywa. Ni mafuta yaliyobarikiwa.

Swali: Ni mamoja yamesomewa au hayakusomewa?

Jibu: Yote ni sawa.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22745/هل-يعالج-السحر-والمس-بزيت-الزيتون
  • Imechapishwa: 13/08/2023