Swali: Tunatakiwa kuchukua msimamo gani juu ya Hadiyth dhaifu zilizotajwa katika baadhi ya vitabu vya wanazuoni?

Jibu: Umejuaje kama ni dhaifu? Wewe umezamilia katika elimu ya Hadiyth? Isitoshe Hadiyth dhaifu zinalingana? Ziko ambazo zinafika katika kiwango cha uzuri, zingine zinafanyiwa kazi katika kupendezesha na kukhofisha. Hili ni jambo la kuwaachia wanazuoni.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (35)
  • Imechapishwa: 11/09/2023