Mtoto wa nje ya ndoa na mwanamke asiyekuwa muislamu

Swali: Mwanaume ambaye ni muislamu amezini na mwanamke asiyekuwa muislamu ambaye akabeba mimba yake. Akasilimu baada ya kumzalia mtoto. Ni ipi hukumu ya mtoto huyu? Anazingatiwa ni mtoto wa ndani ya ndoa?

Jibu: Mtoto hahesabiki ni wa ndani ya ndoa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Mtoto ni wa kitandani. Mzinifu anastahiki [kupigwa] jiwe.”

Mtoto ni mwenye kumwandama mama yake. Mzinzi amekula patupu na anayo majuto.

Hapana vibaya kwake mwanaume kumuoa mwanamke huyo ikiwa anajua kama ametubia. Vinginevyo Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

الزَّانِيَةُ وَالزَّانِي فَاجْلِدُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِّنْهُمَا مِائَةَ جَلْدَةٍ ۖ وَلَا تَأْخُذْكُم بِهِمَا رَأْفَةٌ فِي دِينِ اللَّـهِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ وَلْيَشْهَدْ عَذَابَهُمَا طَائِفَةٌ مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ

“Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamme mpigeni kila mmoja katika wawili hao bakora mia na wala isiwashikeni huruma kwa ajili yao katika hukumu ya Allaah mkiwa kweli mnamuamini Allaah na siku ya Mwisho. Na washuhudie adhabu yao kundi la waumini.”[1]

Bi maana ni haramu kumuoa mwanamke mzinzi au mwanaume mzinzi kumuoa mwanamke anayejiepusha na machafu. Kwa hiyo akijua kuwa ametubu kutokana na uzinzi na amesilimu, basi hapana vibaya akamuoa.

[1] 24:02

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tuhfat-ul-Mujiyb, uk. 60
  • Imechapishwa: 11/09/2023