22. Wakati Mtume alipomuona mwanamke mrembo

11 – Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona mwanamke mmoja akampendeza ambapo akamwendea Sawdah ambaye alikuwa anatengeneza vitu vizuri na kutembelewa na kundi la wanawake. Wanawake wale wakawaacha ambapo akamjamii. Kisha akasema: ”Mwanaume yeyote atakayemuona mwanamke anayempendeza basi amwendee mke wake, kwa sababu yuko na kile kilicho na huyo mwingine.”[1]

[1] ad-Daarimiy kupitia kwa Ibn Mas´uud na Muslim, Ibn Hibbaan na wengine kupitia kwa Jaabir. Ibn-ul-Qattwaan ameisahihisha katika ”an-Nadhwar” (12/18 – muswada). Ahmad pia ameipokea kupitia kwa Abu Kabshah al-Anmaariy. Imetajwa pia katika ”as-Swahiyhah” (235).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 71
  • Imechapishwa: 11/09/2023