10 – Ibn ´Abbaas amesema tena:

”Mwanamke mmoja alikuwa akiswali nyuma yake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Naapa kwa Allaah! Sijawahi kumuona mwanamke mrembo kama yeye. Baadhi ya wanamme walikuwa wakitangulia katika safu ya mbele ili wasimuone, na wengine wanachelewa ili waswali safu ya nyuma. Wanaporukuu, wanaangalia chini ya makwapa yao. Ndipo Allaah (Ta´ala) akateremsha:

وَلَقَدْ عَلِمْنَا الْمُسْتَقْدِمِينَ مِنكُمْ وَلَقَدْ عَلِمْنَا الْمُسْتَأْخِرِينَ

”Tumekwishajua  [vizazi)] vilivyotangulia miongoni mwenu na tumekwishajua wenye kuja baadaye.”[1] [2]

[1] 15:24

[2] Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa’iy, Ibn Maajah na al-Haakim ambaye ameisahihisha na adh-Dhahabiy akaafikiana naye. Shaykh Ahmad Shaakir pia ameisahihisha (4/278), mambo ni kama alivosema. Nimeihakiki katika ”ath-Thamar al-Mustatwaab fiy Fiqh-is-Sunnah wal-Kitaab” na ”as-Swahiyhah” (2472).

Hii ni dalili ya wazi juu ya kosa la Shaykh at-Tuwayjiriy pale anaposoma:

”Mwanamke ambaye anaswali kati ya wanamme wa kando ni lazima kwake kufunika uso wake hata kama anaswali.” (Uk. 170)

Na mfano wake aliyonakili kutoka kwa Ahmad (Rahimahu Allaah):

”Wakati mwanamke anaswali haitakiwi kuonekana kwake kitu hata kucha lake.”

Haiwezekani. Anapswa kuinua mikono yake wakati wa Takbiyr na wakati anapoiweka mahali pake wakati wa Rukuu´, Sujuud na Tashahhud. Maneno hayo yanachenguliwa na maafikiano ya Ibn Battwaal yaliyotangulia.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 71
  • Imechapishwa: 11/09/2023