09 – ´Atwaa´ bin Rabaah amesimulia kuwa Ibn ´Abbaas alimwambia:

”Je, nisikuonyeshe mwanamke wa Peponi?” Nikasema: ”Ndio.” Akasema: ”Mwanamke huyu mweusi. Alimjia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: ”Mimi naugua kifafa na kubaki wazi. Niombee du´aa kwa Allaah.” Akasema: ”Ukipenda kuwa na subira na uko na Pepo, na ukitaka nitakuombea kwa Allaah akuponye.” Akasema: ”Nasubiri. Lakini nabaki wazi. Niombee kwa Allaah nisibaki wazi.” Akamuombea du´aa.”[1]

[1] al-Bukhaariy (10/94), Muslim (8/16) na Ahmad (3240).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Jilbaab-ul-Mar-ah al-Muslimah, uk. 70
  • Imechapishwa: 11/09/2023