15. Hali ya Mtume ilikuwa vipi kabla ya wahy?

Swali 15: Hali yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilikuwa vipi kabla ya wahy?

Jibu: Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akitumia nyusiku kadhaa kwenye pango la Hiraa´ akifanya ´ibaadah. Alikuwa akijichukulia riziki kwa ajili ya jambo hilo. Kisha akirudi kwa Khadiyjah na kuleta tena riziki kiasi hicho. Aliendelea katika hali hiyo mpaka haki ikamjilia akiwa katika pango la Hiraa´.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 95
  • Imechapishwa: 11/09/2023