Swali: Kwa nini elimu imetangulizwa kabla ya matendo? Je, nikitanguliza matendo inajuzu au hapana?
Jibu: Haijuzu kufanya matendo pasi na elimu. Elimu ndio msingi na ndio inasahihisha matendo. Ni lazima ujifunze kwanza ndio ufanye matendo. Allaah (Ta´ala) amesema:
فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ
“Basi jua kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na omba msamaha kwa dhambi zako na za waumini wa kiume na waumini wa kike.” (47:19)
al-Bukhaariy (Rahimahu Allaah) amesema:
“Akatanguliza elimu kabla ya kauli na matendo.”
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/node/1963
- Imechapishwa: 06/09/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)