Ulazima wa kujifunza kwanza kisha matendo baadaye

Swali: Kwa nini elimu imetangulizwa kabla ya matendo? Je, nikitanguliza matendo inajuzu au hapana?

Jibu: Haijuzu kufanya matendo pasi na elimu. Elimu ndio msingi na ndio inasahihisha matendo. Ni lazima ujifunze kwanza ndio ufanye matendo. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَاعْلَمْ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا اللَّـهُ وَاسْتَغْفِرْ لِذَنبِكَ وَلِلْمُؤْمِنِينَ وَالْمُؤْمِنَاتِ

“Basi jua kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah na omba msamaha kwa dhambi zako na za waumini wa kiume na waumini wa kike.” (47:19)

al-Bukhaariy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Akatanguliza elimu kabla ya kauli na matendo.”

Check Also

Darsa na al-Fawzaan au kazi?

Swali: Mimi ni mara yangu ya kwanza ninakaa katika darsa hizi zilizobarikiwa. Kwa kweli nataka …