Ukimcha basi Allaah atakutengenezea mambo yako

Allaah (Ta´ala) amesema:

وَمَن يَتَّقِ اللَّـهَ يَجْعَل لَّهُ مَخْرَجًا وَيَرْزُقْهُ مِنْ حَيْثُ لَا يَحْتَسِبُ

“Na yeyote yuleanayemcha Allaah, atamjaalia njia [ya kutoka katika matatizo] na atamruzuku kutoka njia ambayo hatizamii.” (65:02-03)

Kumcha Allaah kwa kufanya yale aliyoamrisha na kuacha aliyokukataza, basi Allaah humjaalia mtu kama huyu njia ya kutokea juu ya kila zito. Kila jambo ambalo litamkuia zito na yeye ni mwenye kumcha Allaah (´Azza wa Jall), basi atamjaalia njia ya kutokea. Ni mamoja ikiwa ni katika riziki, mali, watoto, jamii na mengineyo. Maadamu unamcha Allaah basi amini kuwa Allaah atakujaalia njia ya kutokea kwa kila zito. Amini hilo. Kwa sababu hii ni kauli ya Yule mwenye kuliambia jambo “Kuwa!” na linakuwa.

Kuna watu wengi waliyomcha Allaah na Allaah akawajaalia njia ya kutokea. Miongoni mwa watu hao ni wale watu watatu ambapo pango liliwafungia.Kuliteremka jiwe kwenye mlango wa pango na likawa limewafungia. Wakajaribu kuliondosha lakini hata hivyo hawakuweza kufanya hivo. Kila mmoja akafanya Tawassul kwa matendo yake mema kumuomba Allaah (´Azza wa Jall). Allaah akawapa faraja na kuwaondoshea jiwe hilo[1]. Allaah akawajaalia njia ya kutokea.

[1] al-Bukhaariy (3465).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/516-517)